Wafanyakazi wakienda kumpongeza Mhandisi Zuhura mara baada ya kwenda kupokea zawadi
Wafanyakazi wakienda kumpongeza Mhandisi Zuhura mara baada ya kwenda kupokea zawadi.
**************
Sikukuu ya Wafanyakazi inayotambulika kama Mei Mosi imekamilika katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo Wafanyakazi wa Taasisi na Mashirika wameshiriki kuadhimisha siku hiyo.
Wafanyakazi wamepewa tuzo mbalimbali kama motisha katika utendaji kazi katika ofisi zao,Mhandisi Zuhura Amani amekua mfanyakazi bora kutoka wakala wa Barabara(Tanroads)mkoa wa Tanga.
Mhandisi Zuhura amesema siri ya mafanikio yake ni kufanya kazi bila kujali muda,muda wote anakua yupo tayari kwa kazi atakayopangiwa na itakayojitokeza.
"Kuwa mfanyakazibora kwa kweli nikufanya kazi kwa muda wote,wakati wowote unapoambiwa kuna kazi unakuwa tayari,kazi zetu sisi Tanroads tunafanya kazi ya matengenezo ya Barabara,huwezi kusema muda wa kutengeneza Barabara ni muda wa siku za kazi,tunafanya kazi hadi zaidi ya muda,barabara zinakatika wakati upo kwenye mapumziko lakini inabidi uende"alisema Mhandisi Zuhura
Pia amewashukuru wafanyakazi wenzake kwa kumchagua kuwa mfanyakazi bora na amewataka wawe tayari kufanya kazi kwa muda wowote inapotokea dharura,ikiwa kazi yao ni kusimamia miundo mbinu ya barabara inayojengwa na wakandarasi.
0 Comments