CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI MWEKA WAFANYA USAFI PANGANI

Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka wameishauri jamii iwe na utaratibu wa mara kwa mara wa kufanya usafi ili kuoka viumbe ambavyo wanaathirika kutokana uchafu utakaokuwa unazagaa hasa nailoni kwenye maeneo ya pembezoni mwa mito au bahari.

Nailoni imekua hatari kwa wanyama jamii ya Ng'ombe na Mbuzi ambapo wakila inaweza kuwasababishia vifo wanyama hao kwa kuwa hazisagiki katika tumbo na ndio imekua uchafu unaozagaa katika maeneo mengi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Profesa Wahabu Kimaro walipokuwa wakifanya usafi pembezoni mwa mto Pangani mkoani Tanga,ikiwa ni kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

"Tunaomba Halmashauri ihakikishe yanaendelea kuwekwa yakiwa safi,Kwa kuwa katika eneo hili kunashughuli mbalimbali za kijamii zinaendelea na Wananchi wapo,mifugo ipo pamoja na takataka,na takataka ni hatari Kwamifugo Kwa kuwa wakila inaziba utumbo"Alisema Profesa 

Ameongeza kuwa ni vema zoezi la kutunza Mazingira liwe endelevu na Wananchi wawe wanashirikishwa na wahimizwe wasitupe taka hovyo.

"Tumefanya zoezi hili na litakua endelevu na tutafanya katika maeneo mengine,na hii ni katika kuadhimisha miaka 60 ya Chuo chetu"alisema Profesa Wahabu

Aidha ameongeza kuwa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka imeendelea kutoa wataalamu katika nchi mbalimbali Duniani,na kwa hapa nchini imetoa  wataalamu zaidi ya Asilimia 70 ni wahitimu wa Chuo cha Mweka wanaosimamia Hifadhi zetu wanaoendesha shughuli za utalii.

Nae Afisa Mwandamizi kutoka chuo hichoAbdon Mallya amesema kuwa nia yao ya kwenda kufanya usafi Pangani,ni kwa ajili ya kushirikisha jamii na kupata uzoefu wa namna wanavyopambana na changamoto kwa vitendo,sisi tunafanya kwa nadharia na wenzetu wanafanya kwa vitendo sasa tukishirikiana kwa pamoja,tunaweza kusaidia jamii kwa kiasi kikubwa"alisema Mallya

Post a Comment

0 Comments