UFARANSA YATAKA AMANI ISRAEL NA PALESTINA

 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili nchini Israel Jumanne Oktoba 24,akiwa na nia ya kufanyia kazi usitishaji vita na kujaribu kupaza sauti ili Ufaransa isikike kwa kuomba suluhu ya mataifa mawili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea uungaji mkono wa Ufaransa kwa Israeli na Wafaransa huko Israeli na kupendekeza kuanzishwa mchakato wa kweli wa amani baada ya shambulio baya la Hamas mnamo Oktoba 7. 

Emmanuel Macron amekuwa akibaini kwamba atafanya ziara nchini Israel ikiwa safari ni muhimu ukanda mzima wa Mashariki ya Kati.

Wakati huu umewadia kulingana na Ikulu ya Élysée.

Macron yuko nchini Israel akiwa na malengo ya kutoa ujumbe wa mshikamano kamili kwa Waisraeli na kwa waathiriwa wa shambulio la Hamas,ambapo atakutana na familia zao.

Post a Comment

0 Comments