WAASI WAIDHIBITI KAMBI YA JESHI MALI

Waasi wa Tuareg kaskazini mwa Mali wanadai kuteka kambi mpya ya jeshi la kitaifa kaskazini mwa nchi, linalokailiwa na mapigano tangu mwezi wa Agosti.

Kundi jingine la Tuareg la baraza la umoja la Azawad-HCUA limebaini katika taarifa yake fupi kwenye mitandao ya kijamii kwamba kambi ya jeshi huko Taoussa, karibu na Bourem katika mkoa wa Gao

HCUA ni mojawapo ya makundi ya Azawad (CMA), muungano wa makundi yenye wapiganaji wengi wa Tuareg ambayo, baada ya kuanzisha uasi dhidi ya serikali kuu mwaka 2012, yalitia saini kwenye mkataba wa amani mwaka 2015 lakini waliamua tena kuchukua silaha mwezi wa Agosti mwaka huu.

Kambi kadhaa za jeshi zimekumbwa na mashambulizi kutoka kwa CMA lakini pia kutoka kwa Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (GSIM), lenye uhusiano na Al-Qaeda, kati ya mikoa ya Timbuktu na Gao, na hata kusini.

Washambuliaji kwa kawaida hudhibiti ngome za jeshi na kuondoka baada ya muda, kulingana na habari adimu na picha zinazotokana na matukio haya. Mamlaka za kijeshi kwa ujumla zinasema kuwa ziliwazuia washambuliaji. Madai ya pande zote hizo ni vigumu kuthibitisha katika maeneo haya ambayo ufikaji wake ni mgumu. Upatikanaji wa vyanzo vya kujitegemea katika mazingira ya uhasama na utawala wa kijeshi ni mgumu.

Tangu mwishoni mwa mwezi wa Agosti, eneo la kaskazini mwa Mali limekuwa uwanja wa mapigano mapya dhidi ya jeshi, katika muktadha wa ushindani wa kudhibiti eneo hilo. Kuibuka tena huku kunafanyika sanjari na kujiondoa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, kufuatia shinikizo la utawala wa kijeshi ulio madarakani tangu 2020. Kuongezeka huku kwa mapigano kumechochewa na vurugu zinazoendelea katika katkati mwa nchi na kuenea kwa wanajihadi kaskazini na mashariki.

Msafara wa jeshi unaojumuisha makumi ya magari ya kivita uliondoka Gao siku ya Jumatatu kuelekea eneo la Kidal, ngome ya waasi wa Tuareg. Vyanzo vya ndani viliripoti urushianaji risasi siku ya Jumatano asubuhi katika sekta ya Tarkint.

Post a Comment

0 Comments