WAZIRI MKUU KHAN MSTAAFU KIZIMBANI KWA KUVUJISHA SIRI ZA SERIKALI

Mahakama maalum ya Pakistan leo imemfungulia mashitaka Imran Khan Waziri Mkuu wa zamani aliyefungwa jela,pamoja na naibu wake kuhusiana na shutuma zenye utata za kuvujisha siri za serikali.

Jopo la mahakama limesikiliza kesi hiyo kwa faragha ndani ya jela iliyoko karibu na mji mkuu wa Islamabad.

Mwongoza mashitaka maalum Shah Khawar aliwaambia wanahabari nje ya jela ya Adiala,kwa mujibu wa sheria ya kikoloni kuhusu siri za serikali,kikao cha kilikuwa cha kuwafungulia mashitaka,ndiyo maana wakasomewa mbele ya mahakama.

Amesema kwamba mahakama imeanza rasmi kusikiliza kesi hiyo na kwamba mashahidi watakuwepo kwenye usikilizaji wa Ijumaa.

Khan mwenye umri wa miaka 70 na mshtakiwa mwenza Shah Mahmood Qureshi ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Pakistan, wamekana mashitaka hayo, mawakili wao wamesema. Wameongeza kusema kwamba wameapa kupinga mashitaka hayo kwenye mahakama ya juu.

Post a Comment

0 Comments