MWALIMU AHUKUMIWA MIAKA 20 MATUKIO YA KIMBARI

Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda imemtia hatiani Wenceslas Twagirayezu, kutokana na kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Watusi nchini Rwanda,miaka 30 iliyopita.

Mahakama hiyo inayoketi mjini Kigali,imeamuru mwalimu huyo kutumikia kifungo cha miaka 20 jela, kutokana na kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994,yalioua zaidi ya watu 800,000.

Mwanzoni mwa mwaka 2024,Mahakama Kuu ilimwachia huru Twagirayezu, maamuzi yaliyokatiwa rufaa na upande wa waendesha mashitaka.

Twagirayezu, alikuwa ni mwalimu katika chuo cha Baptiste Gacuba kilichopo katika wilaya ya Rubavu anatuhumiwa kushiriki katika mauaji ya Aprili ,8,and 9,mwaka 1994,katika maeneo tofauti ya Gisenyi, yakiwemo Busasamana na Gacamena, ambapo Watusi wengi walipoteza maisha.

Post a Comment

0 Comments