MASAUNI AVITAKA VYOMBO VYA USALAMA KULINDA AMANI YA NCHI WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,CGP Jeremiah Katungu(kushoto) cheti cha ushiriki wa Semina Elekezi ya siku mbili kwa Viongozi Waandamizi wa wizara hiyo iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Camillus Wambura(kushoto) cheti cha ushiriki wa Semina Elekezi ya siku mbili kwa Viongozi Waandamizi wa wizara hiyo iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

**************
Na.Mwandishi Wetu,Kilimanjaro

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amevitaka Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo kujiandaa na chaguzi zinazokuja ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani huku akivitaka vyombo hivyo kuacha milango wazi kwa  wananchi wanaofika katika ofisi zao kutoa malalamiko mbalimbali.

Ametoa kauli hiyo mkoani Kilimanjaro wakati akifunga Semina Elekezi kwa Wakuu wa Vyombo vya Usalama,Viongozi Waandamizi na Washiriki wa semina ambapo mada  zilizolenga kuwajenga viiongozi hao waandamizi  ziliwasilishwa na watoa mada kutoka taasisi mbalimbali  za serikali

Wizara hii ina vyombo ambavyo vimebeba taswira ya serikali kwa maana nyingine vimebeba taswira ya wananchi,kwahiyo tukiwa tunayatambua hayo na tukitembea na dhana ya 4R tutaenda kuibeba dhana hiyo hasa kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani kwahiyo mjue kwamba wizara hii ni tegemeo kubwa sana na tuhakikishe tunaingia katika uchaguzi nchi yetu ikiendelea kubaki salama’ alisema Masauni

Waziri Masauni pia alizungumzia suala la malalamiko ya wananchi akivitaka vyombo vya usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo kuhakikisha kila mtu kwa nafasi yake ahakiishe anashughulikia malalamiko ya wananchi na kuyatafutia uvumbuzi na sio kuacha wananchi wanazunguka na malalamiko yao.

Suala la malalamiko hatuwezi kulifumbia macho wananchi wengine ni wanyonge maskini wanadhulumiwa wananyanyasika kwsababu hawana fedha na hawamjui mtu gani wa kumfuata wala hawana vyeo,lazima tujue tuna dhima kubwa sana na tujaribu kujiweka katika nafasi zao hao watu unaenda sehemu usikilizwi,haki yako inapotea kwahiyo natumai kwa kuwa leo mmeyafanya hayo hapa katika mafunzo natumai kila mtu kwa nafasi yake akirudi kituo cha kazi ataenda kutatua malalamiko ya wananchi na kwenye mapungufu tukajirekebishe’ alisema Masauni

Akizungumza wakati wa Ufungaji huo Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Ally Senga Gugu aliweka wazi manufaa ya semina hiyo huku jumla ya mada kumi na sita ziliwasilishwa na washiriki kupata mud awa kuuliza maswali Kwenda kwa watoa mada  huku Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Camillus Wambura akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki huku akitoa ushuhuda wa faida za semina hiyo elekezi imewasaidia katika utendaji wao kuelekea katika utekelezaji wa majukumu yao.

Post a Comment

0 Comments