JENGO LA BUNGE MAREKANI LAVAMIWA

Waandamanaji  wafuasi wa Trump wamevamia jengo la Bunge na kusababisha Makamu rais wa Marekani aondolewa bungeni.

Polisi wa jengo la bunge wameamrisha kufungwa kwa jengo lote, wakieleza sababu za kuwepo na kitisho kikubwa, pale maelfu ya waandamanaji wafuasi wa Rais Trump, kuvamia jengo hilo Jumatano jioni kulalamika dhidi ya utaratibu wa kuidhinisha ushindi wa Joe Biden.

Baraza la Senate lililazimika kuahirisha kikao chake wakati kilipokua kinaendelea na utaratibu wa kuidhinsha kura za wajumbe wa uchaguzi kwa ajili ya Biden.

Makamu rais Mike Pence, aliyekua anaongoza kikao hicho aliondolewa mara moja na walinzi wa usalama wa rais kupitia njia ya chini kwa chini za jengo la bunge.

Picha za video zinazosamba kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Marekani, zinaonesha wafuasi wa Trump wakivuka kwa nguvu uzio wa polisi nje ya jengo la Bunge kuingia ndani na wengine wakizunguka kwnye uwanja wa jengo hilo.

Utaratibu wa kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa rais kawaida ni sherehe ya inayofanyika ndani ya bunge kama hatua ya mwisho ya kuidhinisha rasmi matokeo ya Wajumbe wa Uchaguzi walompatia ushindi Biden hapo Disemba 14, lakini utaratibu huo ulipingwa na wabunge wa chache wa chama cha Republican.

Post a Comment

0 Comments