Wananchi mbalimbali wakiwa wamebeba
jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha
Mvungwe kilichopo Kata ya Songe Wilaya ya Kilindi, Juma Mnyau
wakiupeleka katika makazi yake ya milele.
Mnyau alipoteza maisha baada ya kusombwa na maji yam to Mvungwe
alipokuwa akivuka.
Picha na Dege Masoli.
Shekhe wa Kata ya Songe, iliyopo Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga, Ramadhan
Mtambi akiongoza dua mbele ya jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa
mwenyekiti wa serikali ya Kjiji cha Mvungwe Kata ya Songe, Juma Mnyau
ambae alipoteza maisha kwa kusombwa na maji kwenye mto Mvungwe
alipokuwa akivuka.
Picha na Dege Masoli.
****************
Na Dege Masoli,KILINDI.
WATU watatu wamepoteza maisha baada ya kusombwa na maji akiwemomwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mvungwe kilichopo Kata ya Songe
Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga Juma Mnyau.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana eneo la tukio na kudhibitishwa na
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,ACP Saphia Jongo ni kwamba matukio hayo
yalitokea kwa nyakati tofauti katika Kata ya Songe kwa kipindi cha
wiki moja.
Sambamba na mwenyekiti huyo wengine waliyopoteza maisha kwa mwezi huu
wa february ni mkazi mmoja wa kijiji cha Kingo kilichopo Kata ya
Songe,Erasto Mmeka na mjukuu wake ambaye hajajulikana jina walikufa
maji.
Kwa upande wa Kamanda Jongo alisema tukio la mwenyekiti huyo
lilitokea february 22 majira ya saa kumi jioni wakati alipokuwa
akivuka mto Mvungwe akitoka nyumbani kwake kuelekea kijijini na maji
kumzidi nguvu na kumsomba.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio,mashuhuda
hao walidai kuwa Mnyau alikuwa akivuta mro huo akiwa na mkewe mdogo na
mtoto wake wa kiume aliyetajwa kwa jina la Shaban.
Omar Mpepo aliyedai kushuhudia tukio hilo, alieleza kuwa marehemu
aliondozana na famiilia yake na baada ya kufika kwenye mto huo alimpa
mwanae Shaban baiskeli yake aivushe ng'ambo.
"Unajua Shaban alivuka na baiskeli ile pamoja na mama yake mdogo
(mke mdogo wa baba yake) hadi ng'ambo na wakati akirudi baada ya
kuvusha baiskeli alirudi kuvuka na kutana na baba yake ambaye wakati
huo alirudi kuchukua simu yake aliyokuwa ameisahau kwa mke mkubwa"
alisema Mpepo.
Akieleza kuwa wakati yule kijana anavuka kurudi na kukutana na baba
yake upande wa pili alimtahadharisha baba yake kwamba asivuke kwanza
kwa kuwa maji alipovuka kwa mara ya pili yalionekana kuongezeka kwa
kasi.
Hata hivyo marehemu hakuwa na subra na badala yake aliamua kuvuka na
wakati alipofika katikati ya mto maji yalimzidi nguvu na kumsomba na
pamoja na kujitetea lakini haikuwa na mafanikio na hivyo kuzamishwa.
Aidha Mussa Mangole na Salehe Mgunga walieleza namna walivyopata
taarifa ya simu kutoka kwa mmoja wa watoto wake kuhusu tukio na kwamba
baada ya kufika kwenye eneo la tukio waliamua kuusaka mwili wa
marehemu ambao ulikutwa sehemu inayoitwa Kwangome na kuubeba hadi
zahanati ya kijiji cha Mvungwe.
Naye diwani wa Kata ya Songe, Abuubakari Makengwa alieleza tukio
lingine la kijiji cha Kingo ambapo alisema mfugaji wa jamii ya kimasai
Meka pamoja na mjukuu wake walipoteza maisha ambapo mjukuu
alitumbukia kwenye dimbwi la maji huku babu yaker alipigwa na mawimbi.
Na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Safia Jongo amewaasa wananchi kuwa makini katika wakati huu wa mabadiliko ya hali ya hewa ambapo mvua zimekua zikinyesha.
"Watu wachukue tahadhari na ametoa takwimu za watu waliofariki kutokana na mafuriko kuanzia tarehe 11 Januari na Februari 22 ambapo jumla ya idadi ya watu waliofariki na maji kuwa jumla yake watu sita wamefariki maji katika wilaya ya Lushoto,Korogwe,Muheza,Handeni na Kilindi,na watoto wawili kutoka maafa ya maji.
0 Comments