RAIA WAJITOKEZA KUBORESHA AU KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARIO LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kushoto) akishuhudia mwananchi akiandikshwa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. 

*********
Zoezi la Uboreshaji la Daftarila Kudumu la Wapiga Kura kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora limeingia sikuya pili baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. KassimMajaliwa kulizindua Julai 20,2024 katika uwanja wa Kawawa Mkoani Kigoma.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa TumeHuru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani alipata fursa ya kukaguabaadhi ya vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la mpiga Kura katika Wilayaza Kasulu za Buhigwe mkoani Kigoma na kujionea hali ilivyo vituoni na mwitikiowa watu katika vituo hivyo.

Akizungumzia uboreshaji huo,Kailima  alisema hadi kufikia jana tarehe21 Julai 2024, hapakua na changamoto yeyote iliyojitokeza katika mikoa yote yaTabora, Kigoma na Katavi na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingikujiandikisha lakini pia kuboresha taarifa zao.

Aidha Kailima alivipongezavyama kwa kuweka mawakala katika vituo vya uandikishaji na kuwataka mawakalahao kusaidia utambuzi kwa watu wasio raia wa Tanzania ambao watafika kwaajiliya kuandikishwa.

Kailima alitumia nafasi hiyokuwakumbusha wananchi kuwa sasa zimesalia siku tano kati ya saba zilizopangwa kuandikishawananchi katika mikoa hiyo ya Kigoma, Katavi na Tabora hivyo wananchi wazitumiesiku zilizobaki kujitokeza na kujiandikisha.

Amesema vyama vya siasavinawajibu wa kuwahimiza, wanachama,wapenzi na wafuasi wao kujitokeza kujiandikisha na kuboreshataarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Post a Comment

0 Comments