WANAJESHI WA UFARANSA WASHAMBULIWA MALI.

Wanajeshi wawili wa Ufaransa, ambao walikua katika Operesheni  ya Barkhane nchini Mali, wamepoteza maisha katika shambulizi la bomu lililotokea kwenye magari yao.

Askari mmoja alijeruhiwa katika shambulizi la bomu dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa walioshiriki katika operesheni katika mkoa wa Meneka.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa pole kwa familia za wanajeshi waliopoteza maisha.

Gari la wanajeshi waliohudumia katika mkoa wa Hombori, ambao upo mpakani mwa Burkina Faso na Niger nchini Mali, lilishambuliwa na wengine kupata majeruhi mnamo Desemba 28.

Katika Shambulizi hilo, wanajeshi 3 waliuawa.

Post a Comment

0 Comments