Mchezaji wa BOT aliyetwaa medali ya dhahabu kwa mbio za Mita 5000 na Mita 1500 ni Ester Zakayo akikata upepo katika viwanja vya Tanga Tec.
Kiongozi wa Timu ya BOT Alex Makene akiwa na mshindi wa riadha Mita 5000 na Mita 1500 Ester Zakayo,katika viwanja vya Tanga Tec.
Kiongozi wa Timu ya BOT Alex Makene akizungumza katika viwanja vya Tanga Tec mara ya mchezaji wa BOT kuibuka mshindi.
*********
Timu ya BOT imefanikiwa kuchukua ushindi wa jumla kwa upande wa riadha kwa Mita 5000 na mita 1500 zote wakichukua Ubingwa.
Mchezaji wa BOT aliyetwaa medali ya dhahabu kwa mbio za Mita 5000 na Mita 1500 ni Ester Zakayo ambaye ndiye kinara katika wote walioshiriki SHIMMUTA.
Akizungumza kiongozi wa Timu ya BOT Alex Makene,amesema wamejipanga kushiriki kwenye SHIMMUTA wakiwa na ahadi za kushinda kila hatua wanayofikia.
"Tunashukuru mambo sio mabaya,kwa riadha ni kama mlivyoona wenyewe tumechukua ushindi kwenye mbio za Mita 1500 na Mita 5000"alisema Makene
Makene ameongeza kuwa kwenye mpira wa Miguu na Netball kote wamefuzu katika hatua ya mtoano.
"Kwenye timu ya Footbal tumefanikiwa kuongoza kundi na tumeingia katika hatua ya mtoano ya 16 bora"alisema Makene
Ameeleza mikakati yao nikushinda kwa kila hatua wanayofikia,kwa timu zote za Netball na Football lengo ni kuhakikisha wanabeba ubingwa.
Kwa upande wake Mshindi wa SHIMMUTA kwa Riadha Ester Zakayo amesema siri ya ushindi wake ni mazoezi aliyokua anafanya katika maeneo mbalimbali ya Dodoma.
Ester ameeleza kuwa mazoezi yake amekua akifanya katika mazingira ambayo yalikua yanashabihiana na sehemu atakazokuwa anakuja kukimbilia.
"Mazoezi nilikua nafanya katika uwanja wa jamhuri Dodoma,pamoja na maeneo mengine ya mjini ili kutafuta pumzi ya ushindi,na wakati mwingine nakimbia mpaka chuo cha UDOM ili kujiweka fiti"alisema Ester.



0 Comments