Jumla ya wanafunzi 1,309 wamehitimu masomo katika Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS)wanawake ni 461 sawa na asilimia 35 ya wahitimu wote.
Hata hivyo chuo kimesema bado kinaendelea na mpango wake wa kuwezesha wanafunzi wa kike kujiunga na chuo hicho ili kuwe na asilimia sawa kati ya wahitimu wa kike na kiume.
Makamu Mkuu wa MUHAS, Appolinary Kamuhabwa amesema hayo jana Disemba 5,2024 wakati wa mahafali ya 18 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema katika mwaka wa masomo 2024/2025 chuo kimedahili wanafunzi 235 huku walioomba na wenye sifa wakiwa 5,243 hivyo changamoto kubwa ya kinashindwa kudahili wanafunzi wengi ni kutokakana na kukosekana kwa miundombinu ya kufundishia.
"ongezeko la wanafunzi wanaohitaji kusoma katika programu mbalimbali za afya katika chuo kikuu chetu bado linaendelea kuwa changamoto kubwa katika udahili wa wanafunzi mfano katika mwaka wa masomo wa 2024/2025 kati ya waombaji wenye sifa za kujiunga na Muhas 5,243 waombaji 235 katika fani ya udaktari wa binadamu ndio waliopata nafasi sawa na asilimia 4.5 huku walibahatika kuchaguliwa kwenye fani ya ufamasia wakiwa 101 kati ya waombaji 4,842 wenye sifa za kujiunga sawa na asilimia 2", amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha MUHAS Dkt. Rehema Horera amesema mapato ya ndani ya chuo bado hayajafikia kiwango cha kutosha kuendesha shughuli za chuo kwa ufanisi bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
Amesema katika kulifanya hilo, chuo kimebuni miradi ya kuongeza rasilimali fedha ambapo katika mwaka huu Chuo kimepitisha mpango wa kuzalisha pesa ( MUHAS Business Development Plan) ili kuweza kujiendesha.
"Lengo kubwa la mikakati hii ni kuongeza upatikanaji wa fedha ili kuboresha maslahi ya watumishi, Miundombinu ya kufundushia na kujifunza, tafiti, bunifu na shughuli za utawala.
Aidha Dkt. Horera amesema, February 29, 2025 chuo kitafanya kongamano la kumuenzi aliyekuwa Mkuu wa Kwanza wa chuo hicho Hayati Dkt. Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia Mei 29, 2024 kwa kwa mchango mkubwa aliotoa kwa maendeleo ya MUHAS.
"Maandalizi ya kongamano hilo maalamu la kuadhimisha mwaka mmoja wa maisha ya Dkt. Mwinyi yameanza, kongamano hili muhimu litafanyika Februari 29,2025 na litakuwa linafanyika kila mwaka Mwezi Mei ambao ndio mwezi aliozaliwa Dkt. Mwinyi".
.jpeg)

0 Comments