WAZIRI MKUU DKT.MWIGULU AKUTANA NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 20, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Emmanuel Tutuba, katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mlimwa jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi na kifedha, ikiwemo hali ya uchumi wa nchi, mwelekeo wa sera za fedha, pamoja na mchango wa Benki Kuu katika kuimarisha ustahimilivu wa uchumi wa taifa.

Katika kikao hicho, Dkt. Mwigulu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na Benki Kuu ya Tanzania katika kusimamia uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei na kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa uwekezaji na biashara.

Kwa upande wake, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Emmanuel Tutuba, ameeleza juhudi zinazoendelea kufanywa na BoT katika kusimamia sera za fedha, kuimarisha sekta ya fedha na kuhakikisha uthabiti wa mifumo ya kifedha nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Serikali wa kufanya vikao vya ndani na viongozi wa taasisi muhimu za kiuchumi, kwa lengo la kuendelea kusimamia uchumi wa nchi kwa ufanisi na kufikia malengo ya maendeleo ya taifa.

Post a Comment

0 Comments