JESHI LA NIGERIA LAWANAUA MAGAIDI 40 WA BOKO HARAM KATIKA MASHAMBULIZI YA ANGA

Jeshi la Nigeria limesema limewaua angalau magaidi 40 wa Boko Haram katika operesheni za anga zilizofanyika kwa siku mbili mfululizo mapema wiki hii katika jimbo la Borno, kaskazini-mashariki mwa nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili na msemaji wa Jeshi la Anga la Nigeria, Ehimen Ejodame, mashambulizi hayo ya anga yalitekelezwa siku ya Alhamisi na Ijumaa yakilenga ngome za kundi la Boko Haram.

Ejodame amesema katika operesheni hizo, magaidi wasiopungua 40 waliuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa, hali iliyodhoofisha uwezo wa kundi hilo kuendesha mashambulizi katika eneo hilo.

Nigeria imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya Boko Haram na makundi mengine yenye misimamo mikali tangu mwaka 2009. 

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu na kuwafanya mamilioni ya raia kuyahama makazi yao nchini humo pamoja na katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger.

Post a Comment

0 Comments