DKT.MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA ZAMBIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 16, 2026, ameongoza kikao cha kimkakati kilichowakutanisha Mawaziri, Naibu Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa sekta mbalimbali, kilichofanyika Ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili kwa kina changamoto zinazoathiri biashara kati ya Tanzania na Zambia, kwa lengo la kubaini fursa, kuondoa vikwazo na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Wizara zilizoshiriki kikao hicho ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Post a Comment

0 Comments