Vijana Watajwa Nguzo ya Ushindi CCM Tanga

 



TANGA

Mmoja wa vijana wanaoonyesha kujitolea kwa dhati katika kuhakikisha ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025–2030, Mh.Saidi Mohamed,ametajwa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na juhudi zake za kizalendo na mapenzi kwa chama.

Saidi,ambaye ni kijana kutoka Jiji la Tanga, amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa CCM katika nafasi mbalimbali.

Akiwa kwenye kampeni eneo la Makorora,Saidi alionekana akimuombea kura Mh. Rais Dkt.Samia, Mgombea Ubunge wa Tanga Mjini Mh.Kassim Mbaraka,na wagombea wa nafasi za udiwani, ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kuiunga mkono CCM kwa maendeleo endelevu ya jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wananchi walimpongeza kijana huyo wakisema amekuwa mfano wa uzalendo na uongozi bora unaojali maendeleo ya jamii.

“Saidi ni kijana wa watu, amejitoa kwa moyo mmoja kuhakikisha Tanga inabaki ngome imara ya CCM. ameacha shughuli zake nyingi jijini Dar es Salaam ili kuungana nasi kuhamasisha wananchi,” alisema mmoja wa wakazi wa Makorora.

Wananchi wameendelea kupongeza juhudi za vijana kama Saidi ambao wamekuwa wakijitolea bila kuchoka katika kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao.

“Tunatambua juhudi zako,mjomba usichoke,Chama kinahitaji vijana kama wewe wenye moyo wa kizalendo,” alisema mkazi mwingine wa Tanga.

Post a Comment

0 Comments