Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus amesema kuanzishwa kwa NMB Business Club ni kuwafanya wateja wao wawe karibu nao lakini kupitia huko wanapata fursa ya kusikia changamoto mbalimbali za wateja wao na hivyo kuwasaidia kufanya maboresho katika huduma ambazo wamekuwa wakizitoa.
“Ni matumaini yangu baada ya kusikia mada mbalimbali zitakazotolewa nanyi watapata fursa ya kuwapa maeneo yenu ili waendelea kuyachukua na kuyachakata na kuzipatia ufumbuzi na kujenga NMB na wateja walio imara”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba benki hiyo itaendelea kuboresha huduma zake katika maeneo mbalimbali na sasa wameendelea kuwafikia wateja wadogo wadogo wa kule chini na akaunti za NMB zimeboresha.
“Maboresho makubwa ni kiu ya Benki ya NMB kuendelea kuwa chaguo lako ukitaka kuchagua benki NMB iendelea kubaki kuleta huduma za kibunifu zitakazoleta matokeo chanya kwa wateja wetu”Alisema
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Masoud Ismail akizungumza wakati wa mkutano wa Business Club 2024 uliofanyika Jijini Tanga ambapo alisema wanataka wafanyabiashara wasiuziwe nyumba zao na mali wanazomiliki pindi wanapodaiwa madeni bali iundwe kamati ya madeni kila wilaya itakayowezesha upatikanaji wa fedha zinazodaiwa.
Alisema kwamba kamati hizo zihusishe wafanyabiashara wenyewe kwamba mfanyabiashara amekutana na changamoto badala ya kwenda kuuza nyumba yake deni lipelekewe kwenye kamati ya wafanyabiashara wenyewe kwamba anadaiwa na anatakiwa kwenda kuuziwa nyumba yake wafanyaje na itakuwa ni benki ya kwanza kuwashirikisha wafanyabiashara wenyewe kusaidia kulipa madeni badala ya kuuza nyumba.
0 Comments