VIPAUMBELE VYA MUHEZA MIAKA MITANO IJAYO

Akizungumza katika mkutano huo Mgombea udiwani wa kata hiyo Ali Nyangasa alimshukuru Rais na mbunge huyo kwa kuwaondolea adha ya kero ya maji ambapo awali walikuwa wakinywa maji yenye chumvi lakini Sasa wanapata maji safi na salama.

Alisema kuwa kata hiyo imepata miradi wa shilingi bilioni 1.4 ambao ukikamilika utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi ambao hawakuwa na maji katika kipindi cha miaka mingi.

Aliomba katika miaka mitano ijayo wasaidie wananchi wapate mashamba kwa ajili ya kilimo katika lililokuwa shamba la mkonge la Bwembwera.

Alitaka wananchi wasipepese macho wakamchague Rais Samia Suluhu Hassan,mbunge MwanaFA pamoja na yeye kwakuwa wamefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo.

Mgeni rasmi katika mkutano huo Mjumbe wa baraza Kuu Taifa la UVCCM mkoa wa Tanga Biumrah Sekiboko aliwataka wananchi wasiyumbe waende kuwachagua wagombea wa CCM ambao wameweza kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Alisema CCM kupitia mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imeweza kutekeleza ilani yake kwa kupeleka fedha za miradi katika Kila Kijiji.

Alisema katika kata ya Bwembwera wamepata mradi mkubwa wa maji wa Mizembwe wa jumla ya shilingi bilioni 1.4 ambao utakapokamilika utanufaisha vitongoji 18.


* Mradi wa maji Mizembwe unakamilika 

* Ujenzi wa Zahanati ya Mianga ili iweze kutoa huduma kwa wananchi

* Umeme vitongoji Saba vilivyobaki vinamaliziwa na kufanya ujaziliaji katika maeneo mengine

* Ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Bwembwera

* Uchongaji wa barabara ili zipitike mwaka mzima

* Ujenzi wa daraja Kijiji cha Msowero

* Ujenzi wa mahakama kata ya Bwembwera 

* Uchakavu wa shule za msingi Mkului, kihuhwi

* Ujenzi wa ofisi ya mtendaji wa kata Bwembwera 

* Kuongeza nguvu katika utatuzi wa migogoro na 

* Kuhakikisha changamoto zote za kata ya Bwembwera zinakuwa kipaumbele chake.

Post a Comment

0 Comments