DRC na Uganda Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kupitia makubaliano sita yatakayosaidia kukuza biashara,maendeleo na uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kusainiwa siku ya Jumatatu mbele ya Rais wa DRC,Félix Tshisekedi na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, baada ya kikao cha pamoja cha viongozi na mawaziri kutoka nchi hizo kilichofanyika jijini Kampala kuanzia Mei 8 hadi 10.

Maeneo yatakayohusishwa katika makubaliano hayo ni pamoja na usalama wa mipaka, biashara, habari, teknolojia, utalii, uvuvi pamoja na sekta ya kilimo.

Wakati wa mkutano huo, viongozi na mawaziri wa nchi hizo walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa manufaa ya wananchi wa mataifa hayo jirani.

Aidha, DRC na Uganda zimeeleza dhamira ya kujenga vituo vya pamoja vya forodha na masoko ya kisasa katika maeneo ya mpakani ya Kasindi,Bunagana na Mahagi ili kurahisisha biashara na kuongeza shughuli za kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Post a Comment

0 Comments