Safari ya Australia Yasitishwa,Abiria wa MV Hondius Kuelekea Uholanzi

Abiria waliobaki ndani ya meli ya MV Hondius iliyokumbwa na mlipuko wa virusi vya Hanta wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Uholanzi baada ya safari ya ndege ya Australia iliyokuwa imepangwa awali kusitishwa.

Taarifa hiyo imetolewa siku ya Jumatatu na Waziri wa Afya wa Hispania, Monica Garcia, mjini Tenerife ambapo amesema Serikali ya Hispania ilikuwa imeandaa ndege mbili kwa ajili ya kuwasafirisha abiria hao kwenda Australia na Uholanzi.

Hata hivyo, amesema safari ya kuelekea Australia imefutwa baada ya ndege iliyopangwa kushindwa kuwasili kwa wakati uliotarajiwa.

“Hivyo basi, ndege ya Uholanzi itabeba pia abiria ambao walipaswa kusafiri na ndege ya Australia,” amesema Garcia.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, jumla ya watu 54 bado wapo ndani ya meli ya MV Hondius, ambapo abiria 22 wanatarajiwa kushuka kutoka kwenye meli hiyo huku wengine 32 wakisafirishwa kuelekea Uholanzi kwa ndege.

Mamlaka za afya zinaendelea kufuatilia hali ya abiria hao kufuatia mlipuko wa virusi vya Hanta ulioripotiwa ndani ya meli hiyo.

Post a Comment

0 Comments