STAMICO KUWASAIDIA WANAWAKE NA SAMIA KUTUNZA MAZINGIRA NA RAFIKI BRIQUETTES

Mkurugenzi wa wa Shirika la Taifa la Madini Tanzania (STAMICO) Dkt.Venance Mwase akiwekea udongo mche wa mti alioupanda pamoja na Kikundi cha Wanawake na Samia mkoa wa Tanga.

*********
SHIRIKA la Madini la Taifa (Stamico)limesema kwamba agenda yao katika kutunza mazingira sio kupanda miti na kuiacha bali ni kuhakikisha wanaisimamia katika ukuaji wake mpaka inapokuwa mikubwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Mkurugenzi wa wa Shirika la Taifa la Madini Tanzania (STAMICO) Dkt. Venance Mwase wakati akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika eneo la Amboni Jijini Tanga lililoratibiwa na Wanawake na Samia Mkoa wa Tanga lililokwenda sambamba na kutambulisha Nishati Safi mbadala ya Rafiki Briquettes.

Alisema katika agenda hiyo wanazuia pia kukata miti na ili kuizuia lazima kuwa na nishati safi mbadala ya Rafiki Briquettes ambao ni ubunifu uliofanya na shirika hilo katika kuhakikisha suala la utunzaji wa mazingira linapewa umuhimu mkubwa

“Lakini suala la nishati safi ya kupikia ni agenda ya Rais hivyo niwapongeza wanawake na Samia mkoa wa Tanga kwa kuunga mkono agenda hiyo hivyo tutaendelela kuwaunga mkono “Alisema

Aidha alisema kwamba wanawajibu wa kutunza mazingira na kufanya hivyo lazima waangalie nini kinafanya mazingira yanaharibika wananchi wengi bado hawana nishati mbadala bado wanatumia kuni na mkaa ambao unatokana na miti hali ambayo inawafanya kwenda kukata miti ili kupata nishati ya kupikia.

Alisema kwamba programu yao hiyo inakwenda na vitu viwili kwanza hiyo miti inayokatwa wanataka wahamasishe ili ipandwa ndio kitu wanachokifanya  ili kuzuia isikatwe wananchi lazima apike na ale ndio maana wamekuja hiyo nishati mbadala ya kupikia ya Rafiki inatokana na ubunifu na utafiti uliofanywa na shirika la madini la Taifa(Stamico) .

Alisema ili kuhakikisha wanapata nishati mbadala kwa ajili ya wananchi  ambayo ni rafiki kwa matumizi,mazingira na bei kutokana na vipato vyao kwa hiyo wameitamblisha hiyo bidhaa mkoani Tanga .

“Kimsingi utafiti umekamilika na uzalishaji umeanza na namna ya kuuza hiyo bidhaa kundi la wanawake na samia ndio watakuwa wauzaji watakuwa wanazalisha viwandani na watakauokuwa wanaiuza na kuhamasisha matumizi hayo watakuwa ni wakina mama kwa sababu wanakina mama ndio wanaathirika zaidi na utafutaji wa nishati na uchafuzu wa mazingira maana wanasema uchungu wa mwana ni mzazi”Alisema

Alisema kwamba ndio sababu ya kuwapa fursa hiyo ili waunge mkono agenda ya Rais ya mazingira na nishati mbadala ya kupikia lakini hiyo bidhaa impe uchumi huku akieleza kwa kuisambaza haitakuwa kazi ya bure ni ya kibiashara na watawawesha kuwa na kontena na eneo la kuuzia na kuwatangazia na kwenye matukio mbalimbali kama hayo watawasaidia ili kuhakikisha wameweka hamasa kwa wananchi wote waache na kukuata miti na watumie nishati safi mbadala.

Post a Comment

0 Comments