Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro,Jumatatu, Desemba 22, 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamelenga kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), pamoja na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China.



0 Comments