EWURA na TRA Zaimarisha Ushirikiano wa Masuala ya Kikodi

Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamekutana leo, Desemba 23, 2025, na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, hususan katika usimamizi wa masuala ya kikodi yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Gerald Maganga, amesema EWURA itaendelea kuwa mshirika muhimu wa TRA katika kusaidia utekelezaji wa majukumu ya ukusanyaji na usimamizi wa kodi nchini.

“Ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili ni nguzo muhimu ya mafanikio yetu ya pamoja. Ni wajibu wetu kuudumisha na kuhakikisha makubaliano tunayofikia yanatekelezwa kikamilifu,” amesema Bw. Maganga.

Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Bw. Pendolake Elinisafi, ameishukuru EWURA kwa ushirikiano mzuri unaoendelea, na kuahidi kuwa TRA itaendeleza ushirikiano huo kwa lengo la kuweka msingi imara wa mafanikio ya taasisi hizo mbili pamoja na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments