Wawakilishi wa Iran na Marekani wameanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Muscat, Oman, yakilenga kujadili mpango wa nyuklia wa Iran na suala la kuondolewa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ijumaa Februari 7, 2026, kwa upatanishi wa serikali ya Oman, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.
Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyyed Abbas Araghchi, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr bin Hamad Al Busaidi, huku Mjumbe Maalumu wa Marekani, Steve Witkoff, akiwasiliana kupitia mpatanishi huyo.
Ajenda kuu ya mazungumzo hayo ni faili la nyuklia la Iran na kuondolewa vikwazo dhidi ya Tehran.
Oman imeendelea kuwa daraja muhimu la mawasiliano kati ya Iran na Marekani, ikilenga kuimarisha diplomasia na kudumisha amani katika eneo la Mashariki ya Kati.
Hadi sasa, matokeo rasmi ya mazungumzo hayo bado hayajatangazwa.
Kabla ya kuanza kwa mazungumzo, Waziri Araghchi alisema Iran inaingia katika majadiliano hayo kwa tahadhari kubwa, akisisitiza kuwa taifa hilo litasimama kidete kulinda haki na maslahi yake.

0 Comments