Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amerejea nchini baada ya kushiriki katika Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026 pamoja na Uzinduzi wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji Afrika (Global Africa Investment Summit – GAIS), uliofanyika katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Mhe. Rais Dkt. Samia alwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akitokea Dubai, tarehe 6 Februari, 2026, na alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

0 Comments