Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) imelaani vikali shambulio la hivi karibuni lililotokea katika uwanja wa ndege wa Kisangani, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na kulitaja kuwa ni tukio la kigaidi.
Kwa mujibu wa tume hiyo, shambulio hilo lilihatarisha usalama wa raia na ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, hususan za haki za binadamu na za kibinadamu.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, tume ilisema:
“Shambulio hilo ni sawa na kitendo cha kigaidi.”
Kikundi cha waasi cha M23 kimeripotiwa kudai kuhusika na shambulio hilo lililotokea mwishoni mwa juma, na kusema kiliharibu ndege iliyokuwa katika uwanja huo.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa utatuma ujumbe maalumu nchini DRC kusaidia juhudi za kusitisha mapigano katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo, kwa lengo la kurejesha amani na usalama.
0 Comments