Naibu Waziri Mmuya ashiriki mkutano wa SADC kuhusu usimamizi wa maafa nchini Zimbabwe.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Kaspar Mmuya amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Sita wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa nchi wanachama wa Southern African Development Community kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Profesa Palamagamba Kabudi.

Mkutano huo unaofanyika mjini Masvingo kuanzia Mei 11 hadi 14, 2026, unalenga kujadili utekelezaji wa programu za kikanda pamoja na mikakati ya kukabiliana na maafa katika nchi za SADC.

Akiwasili nchini humo, Mhe. Mmuya alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Suzan S. Kaganda, ambaye amepongeza ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo huku akieleza kuwa nchi inaendelea kutumia majukwaa ya kimataifa kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta za utalii, kilimo na uchukuzi.

Mkutano huo pia unawakutanisha wataalamu wa masuala ya maafa kutoka nchi 16 wanachama wa SADC pamoja na mashirika ya kimataifa, ambapo Tanzania inapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kuonesha uwezo wake katika mifumo ya usimamizi wa maafa.

Post a Comment

0 Comments